Nuru FM

Ushirikishwaji wa jamii kukuza uchumi

15 October 2025, 1:17 pm

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James akizungumza katika kongamano. Picha na Ayoub Sanga

Na Ayoub Sanga

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kusisitiza umuhimu wa kuanzisha na kuimarisha maeneo ya kimkakati ya kiuchumi, kwa lengo la kuongeza tija na ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za maendeleo ya taifa.

Katika kongamano la kitaaluma lililoandaliwa na Chuo Kikuu Katoliki Ruaha, RUCU, mkoani Iringa kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi — PPPC Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Kheri James, amesema serikali inaamini kuwa kupitia ushirikiano na wadau mbalimbali wa maendeleo, mafanikio makubwa ya kiuchumi yanaweza kupatikana kwa haraka.

Sauti ya RC Kheri

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki Ruaha, Sr. Profesa Chrispina Lekule, ameeleza kuwa elimu bora ndiyo msingi wa kuandaa kizazi chenye uwezo wa kuchochea mageuzi ya kiuchumi na kijamii.

Sauti ya Lekule

Dkt. Mwajuma Hamza kutoka  Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania amesemaKongamano hilo,  limewaleta pamoja wadau kutoka sekta ya umma na binafsi, kujadili njia bora za kufanikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.

Sauti ya Mwajuma

Naye Mkurugenzi wa Wete Security, Lawrence Mwakasala, ameonesha umuhimu wa mahusiano mazuri kati ya sekta binafsi na sekta ya umma katika kukuza uchumi wa kisasa.

Sauti ya Wete

Kongamano hilo limehitimishwa kwa wito kwa taasisi za elimu, sekta binafsi na serikali kuendeleza majadiliano ya pamoja kwa maendeleo endelevu ya taifa.