Nuru FM

Wakamatwa na laini za simu 94 wakitapeli Iringa

15 September 2025, 9:42 am

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi akizungumza na wanahabari. Picha na Hafidh Ally

Watuhumiwa hao walikuwa na line za simu zilizosajiriwa kwa vitambulisho vya watu tofauti tofauti ambazo walikuwa wakizitumia kutapeli wananchi.

Na Hafidh Ally

Jeshi la polisi Mkoa wa Iringa limewakamata Innocent Moshi (30), mfanyabiashara na mkazi wa Tenguru Mkoa wa Arusha na wenzake wawili wakiwa na laini 94 za mitandao mbalimbali ya simu wakizitumia kujipatia fedha kwa njia ya Udanganyifu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi amesema watuhumiwa hao walitumia mtandao wa kijamii wa Facebook wakitumia jina la kampuni ya ‘Silverland Company LTD’ wakijitambulisha kama ni wafanyakazi wa kampuni hiyo ya kuzalisha vifaranga vya kuku iliyopo Ifunda – Iringa.

Sauti ya Kamanda

Kamanda Bukumbi ameeleza kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakitumia majina ya uongo huku wakisambaza namba za simu walizotumia kupiga simu kwa wananchi jambo lililopelekea kufanya operesheni na kuwakamata ili hatua za kisheria zifuate.

Sauti ya Kamanda

Hata hivyo Kamanda huyo amewataka wananchi kuwa makini pale wanapofanya miamala ya kifedha kujiridhisha na uhalali wa biashara wanayotaka kuilipia na ikiwezekana kutoa taarifa polisi ili kudhibiti matukio hayo.

Sauti ya Kamanda