Nuru FM
Nuru FM
10 September 2025, 12:02 pm

Mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi unafanyika kuanzia leo Septemba 10 hadi Septemba 11, 2025
Na Noela Lucas na Stephen Gerald
Ikiwa wanafunzi wa Darasa la 7 Nchini wameanza kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya Msingi, wananchi Manispaa ya iringa wamewataka wanafunzi hao wajiamini ili waweze kufanya vizuri.
Wakizungumza Na Nuru fm baadhi ya wananchi wamesema kuwa wahitimu hao wakitakiwa kuendelea kusoma ili wakumbuke kile walichojifunza.
Aidha wamewataka wazazi kuwapa watoto wao nafasi ya kujisomea na kuwapunguzia kazi katika kipindi hiki ambacho wanafanya mitihani yao.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dkt. Said Mohamed amewataka wasimamizi kuhakihikisha watahiniwa wote wanafanya mitihani kwa muda uliopangwa.
Kwa mujibu wa Baraza la NECTA Jumla ya watahiniwa 1,172,279 wameanza kufanya mitihani yao leo.