Nuru FM
Nuru FM
8 September 2025, 11:03 am

Katika Muendelezo wa Kampeni za kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi CCM kwa wananchi Mkoani Iringa.
Na Ayoub Sanga
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza dhamira ya Serikali yake kujenga jengo la kisasa la Machinga Complex Manispaa ya Iringa kabla ya kukamilika kwa kipindi chake cha sasa cha uongozi.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wakazi wa Iringa kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Samora, Mhe. Samia amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa Serikali wa kuboresha mazingira ya kufanyia biashara, hasa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga.

Mh. Samia amongeza kuwa Manispaa ilifanikiwa kujenza Ofisi za Machinga Mkoa kwa kushirikiana na TAMISEM ambapo lengo kuu ni kuhakikisha wanaondoa changamoto za muda mrefu zinazowakabili wamachinga, zikiwemo uhaba wa maeneo salama ya kufanyia biashara.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa CCM, na Mjumbe wa Halmashuri kuu ya Taifa Mkoa Wa Iringa” Salim Abri Asas amesema kuwa watashirikiana na wabunge wa Mkoa wa Iringa kunadi sera za Mgombea wao ili kupata kura za kishindo.
