Nuru FM

Mwanamke atolewa uvimbe wa kilo 10 Iringa

3 September 2025, 8:28 pm

Jopo la madaktari bingwa wakiongozwa na Dr. Mwakalebela wakifanya upasuaji. Picha na Zainab Mlimbila.

Na Zainabu Mlimbila

Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa imefanikiwa kufanya upasuaji na kutoa uvimbe wenye uzito wa kilo 10 uliokuwa unamsumbua mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 42 aliyeteseka kwa Zaidi ya miaki 5.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa upasuaji huo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dkt. Alfred Mwakalebela, ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, aliyeongoza jopo la wataalamu kufanikisha upasuaji huo ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kufika hospitalini mapema mara wanapokutana na changamoto za kiafya.

Sauti ya Mwakalebela

Aidha Dkt. Mwakalebela amewataka wananchi pale wanapohisi kuwa na changamoto za kiafya kufika hospitali kupata vipimo vya kitaalamu na kuacha kutumia dawa.

Sauti ya Mwakalebela

Kwa upande wake Bi Debora Tweve Mkazi wa Ilula aliyepatiwa huduma hiyo ya kitabibu amewashukuru watalaamu wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa kufanikiwa kumtoa uvimbe huo wa kilo 10 aliokaa nao kwa miaka 5.

Sauti ya Mgonjwa

Mwanamke huyo amekaa na uvimbe huo kwa miaka 5 bila kwenda Hospitali zaidi ya kwenda kwa waganga wa kienyeji kitu kilichopelekea uvimbe huo kuongezeka zaidi mpaka kufikia kg 10.