Nuru FM
Nuru FM
2 September 2025, 11:33 am

Utaratibu wa kuwasaidia watoto yatima imekuwa ni moja ya matendo yanayoleta baraka katika jamii.
Na Joyce Buganda
Jukwaa la Walimu Wazalendo Manispaa ya Iringa limetoa msaada wa Mahitaji muhimu kuwawezesha watoto yatima wanaoishi na kulelewa katika Kituo cha Huruma Center kilichopo Mawelewele Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Akizungumza baada Kukabidhi msaada huo, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Manispaa ya Iringa, Mwalimu Adam Mwampangala, amesema wameweka utaratibu huo kufanya matendo ya Huruma ili kuwasaidia wahitaji na kuwatia moyo wanaopitia Changamoto na magumu mengine ya kimaisha.
Aidha amewataka wananchi kuwatembelea mara kwa mara watoto wa vituo vyenye uhitaji kuwaona na kuwafariji ili wafikie ndoto zao.

Naye, Msimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima Huruma Center, Mwalimu Godlove Mwaibula, Kwa niaba ya Uongozi mzima wa Kituo hicho, amewashukuru Walimu hao Kwa msaada huo Mkubwa na Wenye Tija, ambapo ameeleza kuwa Kituo hicho kinalea watoto yatima, watoto wanaotoka katika Mazingira magumu na watoto waliofanyiwa Ukatili wa aina mbalimbali.