Nuru FM
Nuru FM
28 August 2025, 10:58 am

“Wananchi wanatakiwa kulinda maeneo yao ili mradi huo unapokamilika waweze kunufaika zaidi kiuchumi” RC Kheri.
Na Ayoub Sanga
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, amepiga marufuku rasmi uuzaji holela wa ardhi unaofanywa na baadhi ya wananchi , hususani maeneo yanayozunguka Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mkombozi.
Akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa skimu hiyo Iliyopo Tarafa ya Pawaga Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James alisema kuwa uuzaji huo unahatarisha ustawi wa wakulima wa eneo hilo, ambao ndio walengwa wakuu wa mradi wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 56.
Mwanahabari Wetu Godfrey Mengele ametuandalia taarifa Kamili………….
