Nuru FM
Nuru FM
26 August 2025, 11:56 am

“ACT wazalendo imekuwa na Mwenendo mbaya wa Uongozi jambo lililopelekea Vigogo wa Chama hicho Jimbo la Iringa kung’atuka” Kalama
Na Joyce Buganda
Viongozi Chama cha ACT wazalendo Jimbo la Iringa Mjini wamejivua uanachama wa chama hicho kutokana na mwenendo mbovu unaoendelea miongoni mwa viongozi wa ngazi ya mkoa.
Hayo yamejili baada ya kuonekana kwa kadi feki za Chama katika mkutano wa kumteua Diwani wa Kata ya kihesa ambaye atakiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Vijana Chama cha ACT wazalendo Jimbo la Iringa mjini Dikson Kalama amesema yeye ameamua kujivua na uanachama kwa sababu chama hicho hakina umoja wala ushirikwishwaji.
Baton Larika ni Mweka hazina Chama cha ACT Jimbo la Iringa Mjini amesema amejitoa kwenye chama viongozi hawashirikishwi toka wachaguliwe.
Kwa upande wake Katibu wa ngome ya Wazee Jimbo la Iringa Mjini Petro Kwanga amemtaka mwnyekiti cha chama cha ACT WAZALENDO mkoa wa Iringa Chiku Abwao kuachia nafasi hiyo kwani haiteendei haki nafasi yake.
Hata hivyo Katibu Mwenezi wa Chama cha ACT Wazalendo Jimbo la Iringa mjini Salehe Chande amesema wapo tayari kukabidhi nyaraka zote za chama cha ACT pia kwa sasa hawatakwnda chama chochote cha siasa.