Nuru FM
Nuru FM
21 August 2025, 11:19 am

Barabara ya Mgololo yenye urefu wa kilomita 80 imekuwa chanzo cha vifo, na kusababisha kutokukua kwa uchumi wa wananchi wa eneo hilo.
Na Hafidh Ally
Wananchi wa Tarafa ya Mgololo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wanakabiliwa na changamoto ya Ubovu wa barabara hali inayopelekea wagonjwa kufariki njiani pindi wanapoelekea hospitalini kwa kutumia barabara hiyo.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Kheri James, Wananchi hao wamesema kuwa barabara hiyo kubwa hasa kipindi cha mvua ambapo wagonjwa wanashindwa kufika katika hospitali za Mafinga Mjini kupata huduma za afya.

Wananchi hao wameiomba serikali kutekeleza ahadi ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara juu ya ujenzi wa barabarahi hili kuwaepusha na vifo visivyo na ulazima pamoja na kukuza uchumi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Kheri James amesema kuwa serikali kwa kutambua changamoto hiyo tayari imetenga fedha ili kuanza ujenzi.
Mh. Kheri amesema kuwa barabara hiyo itatengenezwa kwa kiwango cha lami kwa kuwa barabara hizo zipo katika maeneo muhimu ya kiuchumi na kijamii.
