Nuru FM

Likotiko achukua fomu kugombea udiwani Gangilonga

19 August 2025, 12:40 pm

Likotiko Kenyata akichukua Fomu ya kugombea Nafasi ya Udiwani Kata ya Gangilonga. Picha na Adelphina Kutika

Mgombea huyo amechukua fomu kutetea nafasi yake ya Udiwani kupitia CCM baada ya kuongoza Kata hiyo kuanzia mwaka 2020-2025.

Na Adelphina Kutika

Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Gangilonga, Mheshimiwa Likotiko Kenyata,amechukua rasmi fomu ya kugombea tena nafasi ya udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kushinda na kupitishwa na chama hicho katika mchakato wa kura za maoni uliohitimishwa hivi karibuni.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Kenyata amewashukuru wanachama wa CCM Kata ya Gangilonga kwa imani kubwa waliyoionyesha kwake kwa mara nyingine, na kuahidi kuendeleza kasi ya maendeleo ambayo tayari imeanza kuonekana katika kata hiyo.

Sauti ya Kenyata

Aidha, alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wote wa Gangilonga kuendelea kudumisha mshikamano na ushirikiano bila kujali tofauti za kisiasa, akisisitiza kuwa maendeleo yanahitaji ushirikiano wa kila mmoja.

Sauti ya Kenyata

Kwa upande wake Afisa Msimamizi wa uchaguzi Kata ya Gangilonga Witson  Mwinuka amewataka wagombea kuhakikisha  wadhamini wawe wametoka kata husika na wewe wamejiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura.

Sauti ya Afisa Uchaguzi