Nuru FM

Bil 2.3 kujenga barabara ya Pawaga-Izazi

15 August 2025, 9:40 am

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James akizungumza na Wananchi wa Pawaga. Picha na Hafidh Ally

Ujenzi wa barabara ya Pawaga-Izazi utasaidia wananchi kukuza uchumi wao kwa kusafirisha mazao Yao hasa mpunga.

Na Hafidh Ally

Wananchi wa Tarafa ya Pawaga Wilaya ya Iringa wameipongeza serikali kwa kutenga zaidi ya Shilingi bilioni 2.3 katika mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya kuongeza ujenzi wa Barabara ya Pawaga–Izazi kwa urefu wa Km 3.2.

Wakizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James ya kukagua miradi mbalimbali, wananchi wamesema kuwa barabara hiyo imeongeza thamani ya mazao yao na kuimarisha biashara ikiwemo kufikika kwa urahisi na wanunuzi kutoka mikoa jirani, jambo linalochochea ukuaji wa uchumi wa eneo hilo.

Sauti ya Wananchi

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Iringa amesema kuwa fedha zilizotolewa zitawezesha ujenzi wa jumla ya kilomita 8 za barabara kwa kiwango cha lami, hatua inayotarajiwa kuongeza zaidi ufanisi wa usafirishaji na uchumi wa eneo hilo.

Sauti ya Meneja Tarura

Naye Mkuu Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James amewataka kutumia fursa ya miundombinu hiyo kuanzisha biashara na viwanda vidogo ili kukuza uchumi wa Tarafa ya Pawaga na Mkoa wa Iringa kwa ujumla, sambamba na kuitunza barabara hiyo ili idumu kwa muda mrefu.

Sauti ya RC Kheri

Aidha amewataka wananchi wa Pawaga kutoa ushirikiano kwa mkandarasi wa barabara hiyo sambamba na kuchangamkia fursa ya ujenzi wa barabara hiyo kujiinua kiuchumi.

Sauti ya RC Kheri