Nuru FM

Ngajilo ashinda kura za maoni Iringa Mjini

5 August 2025, 11:58 am

Katibu wa CCM Iringa Mjini Hassan Makoba akitangaza washindi wa kura za Maoni Iringa Mjini. Picha na Ayoub Sanga

Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kuwa mchakato huo wa kupata wagombea wa Ubunge utaamuliwa katika vikao vya ndani ya Chama.

Na Hafidh Ally

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia mchakato wake wa ndani wa kura za maoni kwa ajili ya kumpata mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini katika Uchaguzi Mkuu 2025 , kimemtangaza Fadhili Ngajilo Kuwa mshindi katika jimbo hilo.

Katika matokeo yaliyotangazwa na Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Mjini Hassan Makona, amesema kuwa Fadhili Fabian Ngajilo ameongoza kwa kupata kura nyingi zaidi, akifuatiwa na Wakili Moses Ambindwile akiwa na kura 1523 Mch. Peter Simon Msigwa akiwa na kura 477.

Sauti ya Makoba

Makoba amesema kuwa chama ameeleza kuwa bado mchakato wa vikao vya ndani unaendelea hivyo hakuna mshindi mpaka pale Chama kitakapo maliza mcihakato ya ndani na kumtangaza Mgombea rasmi atakaye peperusha bendera ya chama.

Sauti ya Makoba
Fadhili Ngajilo mshindi wa Kura za Maoni Ubunge Jimbo la Iringa Mjini

Kwa upande wake Fadhili Fabian Ngajilo ambaye ameibuka kinara kwa kuongoza kwa kupata kura 1,899 amesema kuwa yeye bado hajawa mshindi bali ni dalili nzuri kuelekea kwenye Mchakato wa Chama kwa ajili ya kumpata mgombea rasmi wa jimbo la Iringa Mjini Kupita CCM.

Sauti ya Ngajilo

Naye Wakili Moses Ambindwile, ambaye ameibuka wa pili kwa kura 1,523, ametoa shukrani na kueleza kuwa licha ya kutoshika nafasi ya kwanza, mchakato huo kwake ni mafanikio makubwa, hasa kwa kuwa ni mara yake ya kwanza kushiriki kwenye mchakato wa ndani wa CCM.

Sauti ya Ambindwile

Fadhili Fabian Ngajilo ameibuka kinara kwa kuongoza kwa kura nyingi zaidi, akipata kura 1,899. Nafasi ya pili imechukuliwa na Wakili Moses Ambindwile aliyepata kura 1,523, huku Mchungaji Peter Simon Msigwa akiibuka wa tatu kwa kura 477, Jesca Msambatavangu Kura (408), Nguvu Chengula Kura (181), na Islam Huwel Aliyepata Kura (136).