Nuru FM

Wafugaji wa kuku walalamikia gharama za chakula

5 August 2025, 9:26 am

Picha ikionesha Kuku wakipata chakula. Picha na Mkulimambunifu.org

Wafugaji wametakiwa kujielimisha zaidi ili kupunguza hasara na kuhakikisha ubora wa kuku wanaowafuga.

Na Hafidh Ally

Wananchi Mkoani Iringa, wanaojihusisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji na wa kisasa, wameeleza kilio chao kuhusu kupanda kwa gharama za chakula cha kuku hali inayotishia kushindwa kufanya shughuli zao.

Hayo yamezungumzwa na , baadhi ya wafugaji wamesema kuwa hali ya sasa ya soko imekuwa changamoto kubwa kwao, kwani bei ya chakula cha kuku imeongezeka kwa kiwango kikubwa, huku mapato yao yakiwa duni.

Sauti ya Wafugaji

Bw. Joshua Ngwale ni Mfanyabiashara wa chakula cha kuku Manispa ya Iringa ameeleza kuwa, wafugaji wanashindwa kufanya utafiti wa kina wa masoko kabla ya kuanza mradi, hali inayowapelekea kuingia kwenye gharama kubwa.

Sauti ya Mfanyabiashara

Naye Mtaalamu wa ufugaji wa kuku Manispaa Iringa Bw. Leonard Mwakalinga amesema kuwa ili kupunguza gharama, wafugaji wanapaswa kuzingatia matumizi ya mbinu za asili na mbadala katika kuandaa chakula cha kuku.

Sauti ya Mtaalamu