Nuru FM

Watia nia Mafinga waonywa kuhusu rushwa

31 July 2025, 11:46 am

Baadhi ya wagombea wa nafasi za Ubunge jimbo la Mafinga wakinadiwa kwa wajumbe wa kura za maoni. Picha na Fredrick Siwale

Rushwa imetajwa kuwa miongoni mwa adui wa haki katika uchaguzi jambo linalopelekea kupingwa.

Na Fredrick Siwale

Wagombea na Wajumbe Jimbo la Mafinga Mkoani Iringa wameonywa kutojihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea kura za maoni na Uchaguzi mkuu.

Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UV CCM) Wilaya ya Mufindi Ndugu Christian Mahenge, wakati kuwanadi Wagombea wa Ubunge kwa Wapiga kura huku aki wataka wajumbe kuzingatia miiko ya Chama Cha Mapinduzi katika mchakato huo.

Sauti ya Mahenge

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Cosato David Chumi ameomba kura za maoni kwa Wajumbe katika kata ya Changalawe Halmashauri ya Mji Mafinga, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa ili kupata ridhaa ya kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi mkuu.

Sauti ya Chumi

Naye Mtia nia Agrey Tonga amesema kuwa anaomba ridhaa ya kupewa nafasi ya kugombea katika jimbo la Mafunga Mjini ili kutumia rasilimali za Mafinga kuwanufaisha wakazi wake katika maendeleo.

Sauti ya Tonga

Chumi ni kati ya watano wanao wania nafasi hiyo kupitia CCM ambao walinadiwa kuomba ridhaa katika hatua ya kura za maoni akiwa sambamba na Dickison Nathan Lutevele, Agrey Naftary Tonga , Mendrad Lutengano Kigola na Dr. Basil Lwisijo Tweve.