Nuru FM
Nuru FM
30 July 2025, 12:08 pm

Wakati baadhi ya watia nia ya kugombea nafasi za uongozi wakilalamika majina yao kutorudishwa, hali hiyo imekuwa tofauti kwa watia nia Iringa Mjini.
Na Hafidh Ally
Siku moja baada ya Chama cha Mapinduzi CCM kitangaza majina ya watia nia ya kugombea nafasi za ubunge katika majimbo yote hapa Nchini, baadhi ya watia nia ya Ubunge jimbo la Iringa Mjini wameridhishwa na Mchakato huo wa kura za maoni.
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa rasmi ya uteuzi huo leo, Ngajilo amesema uteuzi huo ni fursa ya kipekee na ushahidi kuwa chama chake kinaamini uwezo wake wa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uwazi na kwa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Ngajilo amesema endapo atapata ridhaa ya wajumbe, atatoa kipaumbele kwa fursa za kiuchumi, uwajibikaji wa viongozi na huduma bora za kijamii.

Kwa upande wake kuwa uteuzi huo ni matokeo ya imani, nidhamu na utumishi alioutoa kwa wananchi wa Iringa Mjini katika kipindi chake cha uongozi.
Pamoja na Fadhili Ngajilo wengine walioteuliwa na Kamati Kuu kushiriki mchakato huo wa awali kugombea Jimbo la Iringa Mjini ni pamoja na Jesca Msambatavangu (Mbunge anayemaliza awamu ya kwanza), Mch. Peter Msigwa, Wakili Moses Ambindilwe, Islam Huwel na Nguvu Chengula.