Nuru FM
Nuru FM
17 July 2025, 7:35 pm

Halmashauri hiyo imeonesha mfano katika ukusanyaji mapato huku ikitakiwa kuelekeza kasi hiyo katika usimamizi bora wa fedha zinazokusanywa.
Na Hafidh Ally
Serikali imeipongeza Halmashauri Ya Mji Mafinga kwa Kuvuka Lengo Ukusanyaji Wa Mapato kwa Asilimia 120 Mpaka Kufikia Tarehe 30 Juni, 2025.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Kheri James alipokuwa katika ziara ya kujitambulisha kwa watumumishi wa Halmashauri hiyo huku akimpongeza Mkurugenzi Bi Fidelica Myovela kwa kazi nzuri ya kusimamia ukusanyaji mapato.
“ Niwapongeze kwa ukusanyaji mzuri wa Mapato hakika chini ya Mkurugenzi huyu na Mkuu wenu wa Wilaya Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa mnastahili pongezi, kwenye mapato hakika mmeupiga mwingi sina la kusema, sasa nguvu hii ya ukusanyaji wa mapato nataka kuiona kwenye usimamizi bora wa fedha zinazokusanywa. Na kuendelea kusimamia miradi ya Maendeleo “ Alisema RC
Aidha amesema kuwa ushirikiano anaoupata kutoka kwa watumishi wa mafinga mji ndio sababu ya kufanikiwa katika ukusanyaji mapato Huku akimuomba Mkurugenzi Fidelica kuandaa viongozi wengine wenye moyo kama wake katika kuwatumikia wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Mji. Bi Fidelica Myovela amesema kuwa Hlmashauri ilitakiwa kukusanya Bilion 6.6 lakini hadi June 30 walivuka lengo kwa kukusanya Bilioni 8 sawa na asilimia 120.
Myovela alisema kuwa hadi kufikia juni 30 mwaka huu Halmashauri hiyo imekusanya jumla ya shilingi 8,019,473,055.62 ambayo ni sawa na asilimia 120 ya lengo la makusanyo ya mwaka 2024/2025 ambayo ni shilingi 6,676,760.83
Ameongeza Kuwa kati ya fedha hizo zilizokusanywa mapato Halisi ni shilingi 5,584,032.54 sawa na asilimia 121 na mapato fungwa ni shilingi 2,435,440,575.08 sawa na asilimia 118.
Mkuu wa Mkoa wa IRINGA Mheshimiwa Kheri James amezungumza wa Watumishi wa MJI Mafinga kwa mara ya kwanza baada ya Kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt SAMIA Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo.