Nuru FM

RC Iringa akagua soko lililowaka moto

14 July 2025, 8:16 pm

Mkuu wa Mkoa wa Iringa akiwa katika soko la Mashine tatu lililoteketea kwa moto. Picha na Ayoub Sanga

Soko Hilo lililokuwa mashuhuri katika eneo la Mashine tatu liliteketea kwa moto na kuwaacha wafanyabiashara kuwa katika hali ngumu.

Na Ayoub Sanga

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James ameahidi kusimamia mipango iliyowekwa na kamati ya Maafa na majanga yanatekelezwa ikiwemo kuhakikisha biashara zinarejea kama kawaida baada ya soko la mshine tatu kuteketea kwa moto.

Mh. Kheri James ameyasema hayo mara baada ya kufika eneo la tukio kujionea uharibifu uliosababishwa na moto ambao umeharibu mali zote za wafanyabiashara waliokuwa wakifanya shughuli zao ndani ya soko hilo.

Sauti ya Rc Kheri

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Zaina Mfaume Mlawa amesema kuwa wameshawatafutia soko mbadala wafanyabiashara walioathirika na moto huo ili waendelee na shughuli za kiuchumi.

Sauti ya Mkurugenzi

Awali Mrakibu Mwandamizi wa jeshi la Polisi Jackline Mtei ambaye Ni Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Iringa amesema kuwa wanaendela na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo sambamba na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika masoko Mkoani hapa.

Sauti ya Kamanda

Naye Mwenyekiti wa Soko la Mashine Tatu Japhar Sewando Osama ameiomba Serikali kuwasaidia mitaji ili waweze kuanza upya maisha yao ya biashara.

Sauti ya Mwenyekiti Soko