Nuru FM
Nuru FM
9 July 2025, 1:43 pm

Watumishi na watendaji wote Mkoni Iringa wameaswa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii kwa uadilifu na uzalendo.
Na Ayoub Sanga
Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amekabidhi Ofisi kwa Mkuu wa Mkoa mpya ambae ni Kheri James huku akishukuru kwa ushirikiano aliopewa kipindi alipooongza Mkoa wa Iringa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya ofisi Serukamba yaliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mikutano uliopo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa amewaasa watuimshi kufanya kazi kwa bidii, kuwa waadilifu wawapo kwenye maeno yao ya kazi.
Aidha Mkuu mpya wa Mkoa wa Iringa Kheri James amemshukuru Mh. Peter Serukamba kwa uongozi wake kwani uongozi wake umewaachia alama kwa watumishi na wananchi wa mkoa wa Iringa.

Aidha Mhe Kheri James ameahidi kuendeleza juhudi zote ambazo zimekuwepo wakati wote katika usimamizi mzuri kwenye ukusanyaji wa mapato na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa huu
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iringa Benjamin Sitta amempogeza serukamba kwa uongozi wake lakini pia kwa mheshimiwa Kheri James kwa kuachiwa kijiti anamuamini kwani uongozi wake unajulikana.
Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa Peter Serukamba amehudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi minne na kwa sasa ameingia kwenye siasa.
