Nuru FM

MUCE na TPHPA washirikiana kukuza uchumi

3 July 2025, 9:25 am

Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Dkt. Joseph Ndunguru na Profesa Method Samweli, RAS wa MUCE wakipeana mikono baada ta kuingia makibaliano ya Ushirikiano. Picha na Ayoub Sanga

Ushirikiano huo unalenga kujengeana uwezo katika uandishi wa miradi, hatua inayolenga kusaidia taasisi hizo mbili kupata fedha za kuendesha shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Na Ayoub Sanga

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kimesaini mkataba wa ushirikiano na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Tanzania (TPHPA), ili kuimarisha ushirikiano na kukuza uchumi wa taifa kupitia miradi ya pamoja na kuboresha sekta ya kilimo.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini, Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Dkt. Joseph Ndunguru, alisisitiza kuwa mkataba huo ni sehemu ya mkakati wa pamoja wa kukuza uchumi wa nchi, kuimarisha sekta ya kilimo, na kutumia vyema rasilimali zilizopo nchini kwa manufaa ya taifa.

Sauti ya Ndunguru

“Tunaamini kwamba tukishirikiana kwa karibu, tunaweza kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu. Ushirikiano huu utawezesha taasisi hizi kutumia rasilimali za ndani ikiwemo wataalamu na miundombinu kwa ufanisi zaidi badala ya kutegemea msaada kutoka nje,” alisema Dkt. Ndunguru.

Amesema Kuwa kupitia Rasilimali watu zilizopo katika taasisi hizo itasaidia kutumia fursa ya mioundombinu ya maabara kufanya utafiti wa kisayansi, na fursa za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa chuo hicho.

Sauti ya Ndunguru

Kwa upande wake, Profesa Method Samweli, RAS wa chuo hicho , amesema ushirikiano huo utaongeza uwezo wa serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania, hasa katika sekta za afya ya mimea na mazao ya kilimo.

Sauti ya RAS

“Makubaliano haya ni ya kihistoria na yanaonesha kuwa tuna uwezo wa kushirikiana sisi wenyewe kwa kutumia rasilimali za ndani. Mara nyingi tumekuwa na mtazamo wa kutegemea msaada wa nje, lakini leo tunaonyesha kuwa tunapowekeza nguvu zetu, tunaweza kufanikisha mengi kwa manufaa ya taifa,” amesema Prof. Method