Nuru FM
Nuru FM
2 July 2025, 4:30 pm

Na Godfrey Mengele
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Kheri James amewataka viongozi, Wakuu wa Taasisi na wananchi kwa jumla kuendeleza ushirikiano uliopo ili kutekeleza maendeleo pasina migogoro.
Zoezi la uapisho limefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Iringa ambapo pia viongozi kadhaa wa Serikali na CCM wamehudhuria ikiwemo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Salim Faraj Abri (Asas)
Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wakuu walioteuliwa hiv karibuni wilaya ya kilolo na wilaya ya iringa RC Kheri james amesema kwa kipindi alichohudumu kama mkuu wa wilaya ya iringa kabla ya kupandishwa cheo amepata ushirikiano mkubwa hivyo ni vyema kuendeleza ushirikiano huo.
Aidha RC Kheri James amezitaka halmashauri zote mkoani iringa pamoja na mamlaka ya ukusanyaji mapato tra mkoa wa iringa kuendelea kukusanya mapato ili kutekeleza shughuli za maendeleo zilizopangwa.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa iringa kheri james amesema kuwa mkoa wa iringa uko salama na kuwaasha wakuu wa wilaya walioapishwa kutenga muda wa kuwasikiliza wananchi na si kukaa ofisini.
Wakuu hao wa wilaya ni Benjamin Sitta ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Iringa na Estomin Kyando ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Kilolo.