Nuru FM
Nuru FM
30 June 2025, 8:03 pm

Elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ina umuhimu mkubwa kwa jamii katika kujiletea ustawi wake.
Na Joyce Buganda
Shirika la SOS Chidrens Villages na taasisi ya TAI wamekuja kidigitali kwa kutengeneza jumbe zinahusu afya ya uzazi kwa vijana ili kuhamasisha elimu ya afya ya uzazi kwa kundi hilo.
Akizungumza baada ya kikao kazi kilichofanyika katika hospitali ya Wilaya ya Kilolo Afisa Mradi kutoka Shirika la SOS Chidrens villages kwa wilaya ya Kilolo Jesca Kawonga amesema mradi huo unawezesha vijana katika afua ya afya ya uzazi na afua ya uchumi endelevu.

Kelvin Leonard ni mratibu wa mawasiliano kutoka shirika la vijana linalojihusisha na jamii kwa ujumla TAI amesema na wanatumia nguvu ya teknolojia kama vitabu maigizo au masimulizi mbalimbali ili kufikisha ujumbe kwa jamii.
Kwa upande wao baadhi ya wadau wamesema wanashukuru Shirika la SOS na shirika la TAI wanaamini kuwa jumbe hizi kwa pamoja zitakuwa chachu katika kubadilisha fikra na kuigusa jamii kwa ujumla.