Nuru FM
Nuru FM
4 June 2025, 10:04 am

Kambi ya Madaktari bingwa wa Rais Dkt. Samia wameanza kutoa huduma za kibingwa na bobezi katika Mkoa wa Iringa.
Ayoub Sanga
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeanzisha rasmi kambi ya siku tano ya Madaktari Bingwa na Wauguzi bingwa Mkoani Iringa ikiwa ni muendelezo wa mpango wa Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia.
Akizungumza wakati wa kuwapokea madaktari na wauguzi bingwa 34 katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Credinus Mgimba, amesema kuwa ujio wa timu hiyo ni hatua kubwa itakayosaidia kusogeza huduma muhimu kwa wananchi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kupata matibabu.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka wizara ya afya Bi. Upendo Mamchony, ameeleza kuwa awamu hii ya pili inalenga kuwahudumia zaidi ya wananchi 3,000 katika mkoa mzima wa Iringa.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Iringa ya Frelimo Dkt. Hassan Mtani amesema kuwa Wananchi wametakiwa kufika katika hospitali za wilaya zilizotajwa mapema ili kunufaika na huduma hizi ambazo zinatolewa bila malipo.