Nuru FM

Kiswaga atangaza kugombea Isiman, kumstaafisha Lukuvi

3 June 2025, 12:33 pm

Mkuu wa Wilaya ya Monduli Festo Kiswaga akitangaza nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Ismani Mkoani Iringa Picha na Ayoub Sanga

Mbio za kutangaza nia za kugombea nafasi za uongozi zimezidi kushika kasi ambapo Festo Kiswaga ameonesha nia ya kulitaka Jimbo la Ismani.

Na Hafidh Ally

Mkuu wa Wilaya ya Monduli Festo Kiswaga ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Isimani Mkoani Iringa na yuko tayari kumstaafisha endapo atashindwa kustaafu kwa hiari.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Lumilo Hotel Manispaa ya Iringa, Festo Kiswaga amesema kuwa dhamira hiyo imekuja baada ya Mbunge Wiliam lukuvi kutangaza mwenyewe katika uchaguzi wa mwaka 2020 kuwa hatogombea tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.

Sauti ya Kiswaga

Amesema kuwa kwa maslahi mapana ya jimbo la Ismani ni vyema Lukuvi akaacha kugombea kwani Wananchi wa Ismani wameonesha nia ya kumstaafisha kwa lazima katika uchaguzi.

Kiswaga amesema kuwa Mh. Lukuvi aliwahi kumuita Jijini Dodoma mwaka 2022 na kusisitiza kuwa kwa miaka 30 aliyohudumu kama mbunge katika jimbo la isimani inatisha na hatagombea tena.

“aliwahi kuniita Shopers Plaza na kueleza kuwa hatagombea tena na yuko tayari kuwaachia watu wengine kumalizia kazi za ubunge ambazo hazijakamilika, na pia aliwahi kutamka katika kampeni za mwaka 2020, na hata katika vikao vya ndani ya chama, hivyo anapaswa kuheshimu kauli zake na kuacha wengine kugombea” alisema Festo Kiswaga

Katika hatua nyingine Kiswaga amesema kuwa katika jimbo la isimani kumekuwa na vitisho vinavyoendelea kwa wananchi na wale wenye nia ya kugombea na wananchi wamekuwa wakipewa doti za vitenge kwa kutakiwa kumchagua tena lukuvi katika uchaguzi mkuu.

Sauti ya Kiswaga

Akizungumzia Kitendo cha Lukuvi Kwenda kinyume na matamko ya kutogombea tena katika jimbo Ismani, Mh. Kiswaga amesema kuwa Waziri lukuvi amekuwa akiendesha vikao Jijini Dodoma na akiwa na watu zaidi ya 600 kuwaambia nia ya kurudi Kugombea.

Sauti ya Kiswaga

Aidha amemtaka Mbunge Lukuvi kuacha kuwatisha wanaotia nia ya kutaka kugombea katika jimbo la isimani kwani tayari alishatioa tamko la kuwaaga wananchi wake kutogombea tena baada ya kushinda ubunge mwaka 2020.

Sauti ya Kiswaga