Nuru FM

Iringa yawakumbuka wajane

31 May 2025, 1:44 pm

Picha ya wanakamati wa siku ya wajane wakiwa kwenye kikao Mkoani Iringa. Picha na Editha Maximilian

Mojawapo ya changamoto kubwa wanayokutana nayo wajane ni kukosa mtu wa karibu wa kusaidiana naye kwenye malezi ya watoto na changamoto zingine za kiuchumi.

Na Zaitun Mustapha

Mkoa wa Iringa unajiandaa kuadhimisha siku ya wajane kitaifa huku wananchi wakitakiwa kutowatenga wajane katika jamii.

Akizungumza na katika kikao cha kwanza cha kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo ambayo yatafanyika` ya siku ya wajane yatakayofanyika june 23 2025 Bi Grace amesema kuwa maadhimisho Yatatanguliwa na kongamano tarehe 22 june katika ukumbi wa kichangani.

Sauti ya Grace

Aidha Afisa Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mratibu wa Dawati la Jinsia na Makundi Maalum Fatuma Mohammed ametoa wito kwa wajane na wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo.

Sauti ya Fatma Kutoka Dawati

Nae Mratibu wa Wajane toka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu Bahati Manjwala amesema wizara imeandaa mikakati madhubuti ambayo itaweza kuwasaidia wanawake wajane nchini.

Sauti ya Mratibu

Siku ya kimataifa ya wajane ambayo huadhimishiwa kila Juni 23, mwaka huu imejikita katika kuhakikisha ustawi wa kundi hilo ambalo mara kadhaa hukumbana na mateso katika jamii.

Takwimu zinaonyesha kuwa kuna takribani wajane milioni 259 duniani kote na karibu nusu wanaishi katika hali ya umasikini.