Nuru FM
Nuru FM
28 May 2025, 5:43 pm

Changamoto ya wafanyajasiriamali wadogo Manispaa ya Iringa kuvamia katika maeneo yasiyo Rasmi kufanya shughuli zao imepatiwa mwarobaini.
Na Godfrey Mengele
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imepanga kuanzia masoko mengine kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo ikiwa ni mpango mkakati wa kuhakikisha hawarudi kufanya biashara katika maeneo wasitakiwa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Justice Kijazi wakati wa ukagua wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara walivamia eneo la mashine 3 ambapo amesema kutokana na kundi hilo kukua kila siku ni vyema kujenga masoko hayo ili kuwarahisisha ufanyaji wa biashara zao
Aidha Mkurugenzi Kijazi amesema kuwa hatua zilizochukuliwa kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinalenga kuhakikisha kila mfanyabiashara anafanya biashara bila kikwazo.
Hata hivyo baadhi wafanyabiashara walioondolewa katika maeneo yasiyo rasmi waliyokuwa wanafanyia biashara zao wametaka kusikilizwa ili kubainisha ni maeneo gani nafuu kwao kufanyia biashara mbali na masoko yaliyojengwa