Nuru FM
Nuru FM
20 May 2025, 6:25 pm

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imekuwa na mafanikio katika ukusanyaji wa mapato, ikipongezwa kwa kufanya vizuri.
Na Joyce Buganda
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amelitaka Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kusimamia vyema mapato yanayokusanywa na Halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa kikao Cha Baraza la madiwani kikao Cha robo ya tatu ya kuanzia Mwezi januari mpaka mwezi machi kwa mwaka 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amesema Halmashauri inatakiwa kutekeleza na kumaliza Miradi kwa wakati , kuhakikisha fedha za mikopo zile asilimia 10 zinawafikia walengwa kwa makundi maalumu.
“Madiwani fedha hizi ziwafikie wahusika iwe kwa kutengeneza vikundi awe iwe kwa wale wenye vigezo msitengeneze vikundi vyenu “Alisema Serukamba

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Justice Kijazi amesema wao kama Halmashauri wamekuwa wakifanya vyema kwenye ukusanyaji wa mapato na wataendelea kufanya hivyo kwani Halmashauri imekusanya zaidi ya bilioni 6.5 kuanzia mwezi julai 2024 mpaka mwezi Mei 2025 ambayo ni sawa na asilimia 79.

Hata hivyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amesema watafanya mjadala kujadili sheria ndogo lakini pia wataendelea kusimamia miradi ya maendeleo na kuyafanyia kazi maagizo yote yaliotolewa na mkuu wa Mkoa.