Nuru FM
Nuru FM
20 May 2025, 7:40 am

Na Godfrey Mengele
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba ametangaza rasmi kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu anaenda kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo.
Serukamba ameyasema hayo katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Iringa kilicholenga kusikiliza utekelezaji wa ilani ya chama hicho huku akiwashukuru mwananchi Mkoani Iringa na watumishi kwa kumpa ushirikiano kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yake.
“Mimi leo nadiriki kusema nadhani hii ni Halmashauri yangu ya Mkoa ya mwisho na mimi nimekata shauri namuonea wivu kaka yangu Lukuvi kukaa bungeni muda mrefu na mimi nataka niende hukohuko, na nina uhakika nitashinda huko ninakoenda, nawashukuru sana na wale wote mnaokwenda kugombea nawatakia kila la kheri “
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Daud Yassin amemtakia kila la kheri mkuu huyo wa Mkoa huku akimuelezea jinsi walivyo fanya kazi kwa ukaribu na ushirikiano mkubwa akimtanabaisha kama kiongozi mchapa kazi, mtenda haki na mwenye hofu ya Mungu.
“Serukamba tumeshirikiana nae vizuri sana ni mshauri mzuri, mkweli, kama mnakumbuka aliwahi kusema kitu ambacho hakitaki ni majungu,mtu akienda kwake aende na habari za ukweli tu na kipindi chote ambacho tumefanya nae kazi ushauri wake kwenye chama umekuwa ukitusaidia sana”
Peter serukamba aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa iringa march 09 2024 akitokea mkoani singida ambapo kwa alibadilishana na Halima dendego wakati huo aliyekuwa mkuu wa mkoa wa iringa nay eye kuelekea mkoani singida.
Mpaka sasa serukamba anaondoka mkoani iringa akiwa amedumu katika nafasi hiyo kwa mwaka mmjo na miezi 2