Nuru FM
Nuru FM
22 April 2025, 12:27 pm

Na Adelphina Kutika
Jukwaa la Wanawake Mawakili na Wanasheria “Wowen Inspire Women” (WIW) linalaani vikali tukio la udhalilishaji lililofanywa na kundi la wanafunzi wa kike dhidi ya mwanafunzi mwenzao wa kike kama lilivyoonekana kupitia picha mjongeo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza na vyombo vya habari mjini Iringa Makamu wa Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Laetitia Petro Ntagazwa amesema Wowen Inspire Women ni jukwaa huru lililoanzishwa kwa lengo ni kusaidiana wanawake mawakili na wanasheria kusaidiana kupeana sapoti katika mambo yanayowakabili wenyewe na wanawake nchini
“Tukio hili si tu linakiuka misingi ya utu na heshima ya binadamu, bali pia linaashiria kukosekana kwa maadili, nidhamu, na uelewa wa sheria miongoni mwa baadhi ya wasomi vijana wa leo,” alisema Ntagazwa.
Katika hatua nyingine amepongeza”WIW” kwa hatua za haraka zilizochukuliwa na Serikali kupitia kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, hasa kwa kuhakikisha manusura anapata msaada wa kisaikolojia, kisheria, na kijamii.
Aidha amesema tukio lingine limetokea March 21 2025 katika wilaya mufindi eneo la Bagdadi Mkoani Iringa wanawake wanne walimshambulia mwanamke mwezao na kumjeruhi kupita kiasi kwa tuhuma za wivu wa kimapenzi.