Nuru FM

Wananchi Iringa wamkumbuka Hayati Karume kwa kuuenzi muungano

8 April 2025, 7:47 am

Picha ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Na Zaitun Mustapha na Catherin Soko

Katika kuadhimisha Kumbukizi ya Miaka 53 ya Kifo cha Hayati Abeid Aman Karume, Wananchi Manispaa ya Iringa wamesema ni vyema kuadhimisha siku hii kwa kuuendeleza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Wakizungumza na Nuru FM baadhi ya wananchi Manispaa ya Iringa wamesema kuwa Karume ni kiongozi ambaye ameasisi muungano akishirikina na Hayati Julias Kambarage Nyerere.

Sauti ya Wananchi

Aidha wananchi hao wamesema kuwa Karume alihakikisha watanganyika na Wazanzibar wanashirikiana na hata kuwa na uhuru wa kuishi na kufanya shughuli za kijamii bila kikwazo hivyo ni vyema serikali ikahakikisha kumbukumbu zake zinafundishwa shuleni kwa faida ya vizazi vijavyo.

Sauti ya Wananchi

Mwanahabari wetu Adekphina Kutika amefanya Mahojiaho na Diwani wa Kata ya mkimbizi mh. Eliudi mvela akizungumzia jinsi wanavyomkumbuka hayati Karume.

Sauti ya Mahojiano na Diwani Mvela