Nuru FM

Walimu Mufindi watakiwa kujiepusha na mikopo kausha damu

20 March 2025, 12:27 pm

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi akizungumza katika kikao Cha CWT Mufindi. Picha na Fredrick Siwale

Na Fredrick Siwale

Chama cha Walimu C.W.T Wilaya ya Mufindi Wametakiwa kujiepusha na mikopo umiza na kausha damu,ili kuondoa vitendo vya udhalilishaji wanavyokutana navyo mitaani kutoka kwa Wakopeshaji.

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Dkt.Linda Salekwa akiwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa mkuu wa mwaka wa C.W.T huku akiwataka Walimu kukopa fedha kwenye Taasisi nyingine za kifedha za Serikali au benki yao ya Mwalimu Commercial Bank (MCB).

Sauti ya DC

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa C.W.T. Mkoa wa Iringa Bw.Gaule Andrew Mgalula amesema tatizo la mikopo chechefu, umiza na kausha damu imekuwa ni kero na Janga kubwana limekuwa likiwaletea athari ikiwemo kuuziwa nyumba na mali wanazomiliki.

Sauti ya Mwenyekiti

Amesema kuwa baada ya kuona changamoto za mikopo umiza waliamua kuanzisha benki yao ya Mwalimu Commercial Bank (MCB) ambayo itawasidia kulipa kidogo kidogo.

Sauti ya Mwenyekiti

Naye katibu wa CWT Wilaya ya Mufindi Bw.Patrick Mlowe ,amewataka Walimu kujiepusha na mikopo umiza na badala yake wakope kwenye benki zinazotambuka ili kuondoka na adha za mitaani .

Bw.Mlowe amesema huko mitaani riba inayotozwa ni kubwa sana inayopelekea baadhi yao kadi za benki kuhifadhiwa kwa Wakopeshaji.