Nuru FM

Wanahabari Iringa wakumbushwa kuandika habari za malezi ya watoto

19 March 2025, 11:34 am

Kiongozi wa waandishi wa habari na wasimamizi wa mradi wa PJT MMMAM Iringa. Picha na Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Waandishi wa habari mkoani Iringa wamekumbushwa kuandika ipasavyo habari zinahusu watoto ili kuchochea malezi chanya kwenye jamii.

Akizungunza kwenye mdahalo wa program jumuishi ya malezi,makuzi na mandeleo ya mtoto PJT  MMMAM Mwenyekiti wa Club ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa IPC Frank Leonard amesema  ni vyema wanahabari  wakaibua changamoto zinazowakabili watoto pia kuangalia sera zinazohusu malezi na makuzi ya mtoto na sio kuandika mafanikio pekee.

Sauti ya Leonard

Aidha Leonard amewaomba serikali na wadau wa masuala ya watoto kuwatumia waandishi wa habari ipasavyo kwani waandishi ni daraja la kufikisha ujumbe kwa jamii kwa kutumia vyombo vyao vya habari.

Sauti ya Leonard

Kwa upande wake mratibu wa program hiyo kwa Mkoa wa Iringa Martin Chuwa amesema asilimia 72 ya wananchi wa mkoa wa Iringa wamefikiwa na elimu hii ya malezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto na hii yote ni mashirikiano mazuri yaliopo na waandishi wa habari na program hiyo.

Sauti ya Chuwa

PJT MMMAM  ni program Jumuishi ya Malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto kuanzia miaka 0 mpaka 8 ili lake ni kuleta na kuchochea malezi bora kwa watoto watakapokuwa watu wazima.