Nuru FM

Dkt. Samia aunga Mkono juhudi za wanawake Iringa kwa kukabidhi bajaji

19 March 2025, 11:24 am

Mkuu wa Wilaya ya Iringa akiwa na viongozi wa Dini ya Kiislamu kukabidhi Bajaji. Picha na Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Baraza la Wanawake wa Kiislamu Tanzania, Wilaya ya Iringa wamekabidhiwa Bajaji yenye Thamani ya Shilingi Milioni 10.5 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuunga Mkono Juhudi za Wanawake wa Kiislamu Wilayani humo kukuza uchumi.

Akikabidhi msaada huo Ofisini kwake Kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James amesema kuwa Bajaji hiyo ni  Juhudi za Serikali katika kuwasaidia Wanawake hao kujitengenezea kipato Chao binafsi na Taasisi Kwa Ujumla.

Sauti ya Kheri

Aidha Kheri James ameongeza Kwa kusema Serikali Wilayani humo itaendelea kuunga Mkono Jitihada za Wanawake wote ili kuhakikisha wanajikwamua Kiuchumi.

Sauti ya DC

Kwa upande wake Mlezi wa Baraza hilo Ostadh Mudathir Yoyota amewaasa Wanawake wa Baraza hilo kuweza kukitunza Chombo hicho ili kiweze kuleta manufaa yaliyokusudiwa huku wanawake hao wakishukuru kwa kupatiwa bajaji ili kuwainua kiuchumi.

Sauti ya Mlezi

Zawadi Bajaji hiyo iliyokabidhiwa ni matokea ya maombi maalumu walio yaomba viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo kupitia Kongamano kubwa lililofanyika wilayani Iringa kwa lengo la kuhimiza malezi na maadili kwa watoto ambapo mgeni Rasmi katika kongamano hilo alikuwa Kheri James, Mkuu wa Wilaya ya Iringa.