Nuru FM
Nuru FM
7 March 2025, 6:36 pm

Na Godfrey Mengele
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Kheri James ameitaka Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania – TAWA pamoja na hifadhi ya wanyamapori Ruaha kuchukua hatua madhubuti ili kudhibiti wanyama wanaovamia na kuharibu mazao, mifugo na kusababisha madhara kwa binadamu
DC Kheri James ametoa maagizo hayo kwenye kikao cha ushauri cha Wilaya kilichofanyika Ofisini kwake na kueleza hivi karibuni kuna baadhi ya vijiji vilivyopo karibu na hifadhi na mapori tengefu vimevamiwa na wanyama hao ikiwamo simba na tembo na kufanya uharibifu ambapo ng’ombe 9 zimeliwa .
Kheri James amewataka wananchi kutoa taarifa ikiwa uvamizi wa wanyama utaendelea katika maeneo tofauti na kuziagiza mamlaka husika pindi wapatapo taarifa wazifanyie kazi haraka ili kuzuia madhara makubwa kutokea.
Aidha Kheri James amewataka wananchi kujenga tabia ya kutunza mazingira ili kufanya mfumo wa ikolojia kubaki salama na kuepuka madhara ya wanyama waharibifu wanaovamia na kuharibu mali za watu kama mazao na mifugo
Msikilizaji taarifa hii utaisikia kwa kina hapo baadae ambapo atasikika Afisa tarafa, tarafa ya idodi Ndg Mapesa Makalla akitueleza hatua ambazo wamezichukua ili kukabiliana na changamoto hiyo.
MWISHO