

5 March 2025, 10:15 am
Na Adelphina Kutika
Wanawake Mkoani Iringa wametakiwa kuacha kukopa mikopo ya kausha damu na badala yake wakope mikopo inayotambulika na Serikali ikiwemo taasisi za fedha ili kupunguza vifo kwa vijana.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Rose Ngunangwa , katika Kongamano la Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na shirika la Sauti ya Haki Tanzania na kufanyika katika Ukumbi wa Mwananchi Uliopo Kata Nduli Manispaa Ya Iringa na kuwashauri wanawake wanapokopa wahakikishe wanafanyia malengo yaliyokusudiwa.
Letsia Petro Ntagazwe ni mkurugezi wa shirika la sauti ya haki Tanzania amesema kuwa kama shirika wameona vyema waadhimishe siku ya mwanamke katika kata ya nduli ili kumfikia mwanamke wa chini asiyeitambua haki yake.
Kwa upande wake Paskalina Johel Ipanda Program manager sauti ya haki Tanzania amesema kupitia changamoto zote zilizotolewa katika kongamano hilo zinakusanywa na kufanyiwa kazi ili kutoa suluhisho la kudumu kwa wanawake wa hali ya chini
Nao baadhi ya wanawake waliohudhuria maadhimisho hayo wamesema mikopo kausha damu imekuwa mibaya kutokana na kutumia pasipo malengo hali inayopelekea wanaume kufariki.
Hata hivyo maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2025 yatakuwa kwa namna ya kipekee yakibeba sura ya kipekee kwa kuwa yanaambatana na miaka 30 ya utekelezaji wa Azimio la ulingo wa Beijing (1995) yakiambatana na kaulimbiu isemayo “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”
MWISHO