

21 February 2025, 12:12 pm
Na Fredrick Siwale
Mwalimu wa shule ya msingi Kinyanambo Silvester Joseph Lyuvale (57) aliyepata ajali na kukatwa miguu yote miwili ameiomba Serikali na Wadau wa maendeleo ili aweze kupata msaada wa Kitimwendo kinachotumia umeme.
Akizungumza na Nuru FM Mwl.Silvester anayefundisha ya msingi Kinyanambo Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, amesema kuwa akipata kitimwendo hicho kitamsaidia katika utekelezaji wake wa majukumu yake.
Mwalim Silvester anayefundisha masomo ya Kiingereza na Sayansi amesema kuwa licha ya kupata ulemavu wa kukatwa miguu yote amekuwa akienda shule kufundisha na amekuwa akipitia wakati mgumu kwani kiti mwendo alichonacho hakikidhi mahitaji kufika shuleni kwa wakati.
Bi.Christina Emmanuel Nyakunga Ni mke wa Mwalimu Silvester ameiomba Serikali na Wadau kumsaidia Mume wake ili aweze kuondokana na adha na changamoto anazozipitia pindi anapotaka kufanya kazi za kitaaluma.
Hali ya Uchumi wa Mwalimu Huyo imezidi kuwa mbaya jambo kuishi maisha ya kuunga unga ikiwa ni pamoja na kugonga kokoto na kuuza ili kujikimu huku atakayeweza kumsaidia awasiliane naye kupitia namba 0763-368384.
MWISHO