Nuru FM

Waombwa kuwasaidia wenye uhitaji Iringa

18 February 2025, 8:54 pm

Msanii Ezenice wa Iringa akiwa katika zoezi la kutoa misaada kwa watoto wenye uhitaji. Picha na Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Wadau wa maendeleo mkoani Iringa wametakiwa kuwa na utaratibu wa  kujitoa  na kuwasaidia watu wenye uhitaji na kutowatenga.

Hayo yamzungumzwa na msanii kutoka nyanda za juu kusini Ezra Francis maalufu kwa jina la Eze Nice ambae ndiye alikuwa muandaaji wa tukio hilo wakati wa sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa MNEC Salim Abri katika kituo cha kulelea watoto wenye mazingira magumu cha  Amani kilichopo kata ya kitwiru  na kuongeza na kusema vitu vyenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni moja vilitolewa kituoni hapo ili kurudisha tabasamu kwa watoto hao.

Sauti ya Ezenice

Kwa upande wake mwenyekiti mstaafu wa UVCCM wilaya ya Iringa mjini aliekuwa mgeni rasmi wa tukio hilo  Salvatory Ngelela amesema lengo kubwa la tukio hilo ni kumuunga mkono MNEC Salim Abri ASAS kwa mchango mkubwa wa kimaendeleo anaofanya katika mkoa wa Iringa

Sauti ya Ngerela

Hata hivyo Meneja wa kituo cha kulelea watoto weny mazingira magumu Amani  Elizabeth  Mwakabanga amesema wanashumkuru MNEC kwa kuwasaidia kwani changamoto kubwa iliopo kituoni hapo ni vya mahitaji ya kila siku kama sukari, mafuta ya kula nyakula na vifaa vya shulenu ambavyo ndivyo walivoletewa.

Sauti ya Meneja

MWISHO