Nuru FM

Bi. Mwanilwa akabidhi mifuko 30 ya saruji na mawe ujenzi nyumba ya UWT

9 February 2025, 3:57 pm

Mwanilwa akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Wilaya ya handeni. Picha na Shaffih Mhina

Na Mwandishi wetu

Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga umeanza utekelezaji wa ujenzi wa nyumba ya Watumishi hasa Katibu umoja huo.

Katika ujenzi huo ambao umeanza Rasmi, baada ya kupatikana Vifaa vya ujenzi kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo, Mjumbe wa Mkutano Mkuu UWT Taifa Wilaya ya Handeni Bi Mariam Mwanilwa amechangia Simenti Mifuko 30 na Mawe Trip 3 ambazo zimeshafikishwa katika eneo la Mradi wa ujenzi huo.

Akizungumza wakati wa ufuatiliaji wa Maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo, Bi Mwanilwa amesema kuwa kukamilika kwa nyumba hizo itakuwa ni chachu ya kiongozi huyo kufanya kazi za Chama kwa ufanisi.

“Mimi nimeamua kuunga mkono juhudi za Rais wetu Dkt. Samia Suluhu, katika kuhakikisha tunakuwa na Nyumba ya Watumishi wa UWT kwa kuchangia kidogo nilichojaaliwa Leo yaani Cement Mifuko 30 na Mawe Trip 3” Alisema Mariam Mwanilwa

Naye Katibu wa UWT Wilaya ya Handeni Bi. Asha Muya amewashukuru wadau Wote waliochangia ujenzi huo akiwemo Mariam Mwanilwa, Mbunge wa Handeni Mjini Reuben Kwagilwa, Madiwani wa Wilaya ya Handeni kwa kufanikisha zoezi la ujenzi ambapo kwa Sasa wanaendelea na kuziba shimo la Choo na ujenzi mwingine.

Akizungumzia kuhusu ujenzi huo, Balozi wa Maji Mkoa wa Tanga Habib Mbota Maarufu Moja kwa Moja aliwataka wadau Wengine wa Maendeleo kuchangia ujenzi wa nyumba hizo za 2 wa umoja huo.

” Kwa kweli tunashukuru kwa Moyo wa Mama yetu Mariam kwa kuja kuchangia Mradi huu maana alianzia kuwasaidia watoto Yatima kuwapatia Bati akaona ni vyema pia kupitia huu Mradi na kutoa mchango wake” alisema Mbota.