Nuru FM

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi yapaa ukusanyaji mapato

5 February 2025, 12:08 pm

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh.Festo Mgina, Katibu Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ruben Chongolo Na DED wa Mufindi. Picha Fredrick Siwale

Na Fredrick Siwale

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka imeonyesha kupaa katika ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyanzo vyake mbali mbali vya mapato na kukusanya milioni 170 kwa wiki.

Awali akifunga Baraza hilo Katibu tawala Wilaya ya Mufindi Ruben Chongolo aliwataka Waheshimiwa Madiwani kusimama kidete kusimamia miradi yote na kuhakikisha inasimamia vyanzo vyake vya mapato ya ndani ili kufikia lengo la Sh.9.bilioni na milioni 300 walizokusudia kukusanya kwa mwaka.

Sauti ya DAS

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh.Festo Mgina amempongeza Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya na timu yake kwa kuwajibika huku akiwataka Madiwani kuhakikisha wanatembelea miradi yote ya maendeleo katika maeneo yao ili kuongeza usimamizi na tija kwa Wananchi.

Sauti ya Mwenyekiti

Wakichagia katika baraza hilo baadhi ya madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wamesema kuwa ni vyema wakajifunza kutoka sehemu nyingine ili waweze kuandaa kodi inayoendana na mnyororo wa thamani.

Sauti ya Madiwani

Madiwani na walitoa michango yao ikiwepo suala la uchenjuaji wa madini na huduma za afaya na kushauri elimu itolewe zaidi ili kuhakikisha hakuna mapato yanayo vuja kwa kutozwa Kodi kidogo tofauti na kinachozalishwa.

Naye Mkurugzenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Bw.Mashaka Mfaume ameliambia Baraza la Madiwani kuwa kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba 31 mwaka 2024 Halmashauri imekusanya kiasi cha Sh.170 milioni kwa wiki kutoka milioni 80 kwa wiki kipindi kilichopita .

MWISHO