

5 February 2025, 11:48 am
Na Joyce Buganda
Wadau wa mahakama mkoani iringa wametakiwa kutenda haki wanapokuwa katika majukumu yao ikiwemo kujenga ukaribu kwa wananchi wakati wa wanapotoa huduma za kimahakama.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria yaliofanyika katika viwanja ya mahakama mgeni rasmi wa maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa iringa Peter Serukamba amesema jamii pamoja na wadau wa mahakama washirikiane kwa pamoja katika kutokomeza rushwa haki itendeke.
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili TLS kanda ya Iringa Moses Ambindwile amesema mawakili wa kujitegemea wamekuwa wakipata changanoto nyingi ikiwemo kupewa maneno makali mbele za wateja wao kutoka kwa wadau wa mahakama.
Kwa upande wake jaji mkuu mahakama kuu kanda ya Iringa Dustan Ndunguru amesema maadhimisho hayo yalijumuisha utoaji wa elimu kuhusu sheria kupitia vyombo mbalimbali vya habari kama radio, television ana kwa ana.
Ikumbukwe kauli mbiu ya mwaka huu inasema Tanzania 2050 nafasi ya Taasisi zinazosimamamia haki, madai katika kufikia malngon makuu ya Dira ya Taifa ya maendeleo.