Nuru FM

Takukuru Iringa yabaini kasoro miradi ya maendeleo

28 January 2025, 3:16 pm

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Iringa Domina Mukama akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Hafidh Ally

Na Hafidh Ally

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa Takukuru Mkoa wa Iringa imebaini kasoro katika mradi wa maji wenye thamani ya Bilioni 1.5 fedha za Mfuko wa Maji wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Iringa Domina Mukama amesema kuwa katika kipindi Cha Mwezi October mpaka Dec 2024 Takukuru iliendelea na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za uma katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika vijiji vitano vya Kata ya Sadani Wilaya ya Mufindi.

“Tulibaini kuwa Kampuni ya M/S BEJAN BUSINESS ENTERPRISE ndiyo inayotekeleza Mradi wa Maji Sadani-Kihata katika Kijiji Cha Tambalangombe wenye thamani ya Bilioni 1.5 fedha za Mfuko wa Maji wa Taifa (National Water Fund) kuwa Mkandarasi alishalipwa kiasi Cha Bilioni 1.067 sawa na asilimia 71 ya utekelezaji wa Mradi huo uliofikia asilimia 90.” Alisema Domina

Sauti ya Takukuru

Aliongeza kuwa Takukuru ilibaini kuwa Mabomba ambayo yamepasuka ni yale yaliyounganishwa kwa Watumiaji wa majumbani na kazi hiyo haikufanywa na Mkandarasi M/S BEJAN BUSINESS ENTERPRISE Bali ni msimamizi wa Mradi kutoka chombo Cha Watumiaji maji ngazi ya Jamii CBWSO na sababu ni kutumia Mabomba daraja B badala ya C Kama inavyoelekezwa na Iruwasa.

Pia Takukuru ilibaini sababu nyingine ni Mabomba kutokazwa vizuri kutoka njia kuu kwenda kwa Watumiaji wa majumbani na kusababisha uvunjaji wa Maji.

Sauti ya Takukuru

Katika Hatua nyingine Takukuru ilifuatulia miradi yenye Thamani ya Bilioni 16.064 na imebaini mapungufu katika miradi mitatu yenye thamani ya Bilioni 1.23 katika sekta za Maji, Afya na elimu huku Ikitoa ushauri kufanyiwa marekebisho ambayo yameleta tija na miradi hiyo ipo katika Hali nzuri.

” Katika Mradi wa ujenzi WA Maternity Complex katika hospital ya Mji Mafinga wenye thamani ya Milion 500 ilibainika Kuna sehemu mafundi walikosea kuweka marumamu na baada ya Takukuru kufika tulishauri na maboresho yamefanyika na ujenzi Iko katika Hatua nzuri za ukamilishaji wake” Alisema Mkuu wa Takukuru

Sauti ya Takukuru

 
Hata hivyo Takukuru imesema kuwa inaendelea kutoa elimu ya kupambana na Rushwa huku wananchi na Taasisi Zote wakitakiwa kutoa taarifa pindi wanapona Kuna viashiria vya Rushwa.