Mbunge Kabati akabidhi baiskeli kwa mwenye Ulemavu Ibumu
12 January 2025, 11:37 am
Na Mwandishi wetu
Watu wenye ulemavu mkoa wa Iringa wameendelea kunufaika na jitihada za mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa, Mh Dr. Ritta Kabati za kutoa vifaa saidizi katika kundi hilo.
Kabati ameendelea kutoa vifaa saidizi kwa kukabidhi baiskeli kwa Jaluo Mpalanzi mwenye ulemavu kutoka kata ya Ibumu, Wilaya ya Kilolo.
Kabati amesema watu wenye ulemavu wanamahitaji mengi ikiwepo vifaa saidizi na matibabu ya kiafya na hivyo ameamua kusaidia upatikanaji wa vifaa hivyo ili kuwasaidia kufanya shughuli zao.
Ametoa wito kwa watu wenye ulemavu kusaidiwa katika mchakato wa kupata mikopo ya halmashauri ili kuweza kufanya biashara zao.
Kwa upande wake, ndugu wa Jaluo Mpalanzi aliyepokea baiskeli amemshukuru Mbunge Ritta Kabati kwa kumsaidia Jaluo Mpalanzi kupata baiskeli hiyo.
MWISHO