Wananchi 4,610 wapatiwa msaada wa Kisheria Iringa
24 December 2024, 8:55 am
Na Godfrey Mengele
Takribani wananchi 4,610 wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamefaidika na kampeni ya Msaada wa kisheria ya mama Samia iliyokuwa na lengo la kuwasaidia wananchi utatuzi wa kisheria wa masuala mbalimbali
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Kheri James wakati wa hitimisho la siku 10 za kutoa huduma hiyo ambapo amesema kuwa Migogoro mbalimbali ikiwemo ya Ardhi, Mirathi, Ndoa na Mingine imetatuliwa Kupitia Kampeni hiyo.
Moses Ambindwile ni Mwenyekiti wa Chama cha mawakili Tanganyika TLS amesema kuwa wakati wa kutoa huduma hiyo miongoni mwa mambo waliyokumbana nayo ni changamoto ya mirathi kwa wakazi wa manispaa ya iringa.
Edick Shekizela wakili wa serikali kutoka Wizara ya Katiba na sheria na Mratibu wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Mkoa wa Iringa amesema kuwa pamoja na kufika tamati kwa kampeni hiyo lakini huduma hiyo itaendelea kutolewa kupitia madawati yaliyoanzishwa katika ofisi za halmashauri nchi nzima.
MWISHO