Nuru FM

Skimu ya umwagiliaji Tarafa ya Pawaga kuongeza uzalishaji wa mpunga

4 December 2024, 12:03 pm

Mhandisi wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji Mkoa wa Iringa Mhandisi Peter Hakunai akizungumza kuhusu skimu ya umwagiliaji. Picha na Adelphina Kutika

Na Adelphina Kutika

Ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi wenye thamani ya shilingi bilioni 55 uliopo Tarafa ya Pawaga wilaya ya iringa unatarajia kuongeza uzalishaji wa mpunga na kuinua uchumi wa Kata za Itunundu na Mboliboli.

Hayo ameyasema Mhandisi wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji Mkoa wa Iringa Mhandisi Peter Hakunai,wakati wa ukaguzi wa skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi iliyopo Tarafa ya Pawaga  wakati akitoa ripoti ya mradi huo katika jukwaa la mafanikio la Wilaya ya Iringa

Sauti ya Mhandisi

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji Mkombozi, Abdalah Hamadi Nguso, amesema mradi huo utakuwa chachu kubwa ya kuongeza kipato kwa wakulima, hasa kwa kuwa utaongeza ajira za moja kwa moja na kuimarisha uchumi wa jamii za vijijini.

Sauti ya Mwenyekiti

Naye, Bi. Malietha Sales Luvanga, mmoja wa wakulima wa eneo hilo la Pawaga, amesema kuwa mradi huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa kupata mazao ya kutosha, yatakayochochea uchumi wao.

Sauti ya wakulima

MWISHO