CCM Mufindi yawanadi wagombea wake
21 November 2024, 11:44 am
Na Fredrick Siwale
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimeanza kuwanadi wagombea nafasi uongozi wa Serikali za Mitaa kwa Wananchi kuelekea uchaguzi utakaofanyika Nov 27 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni katika Mtaa wa Mjimwema uliopo Kata ya Boma Diwani wa Kata hiyo Mh.Julist Kisoma aliwaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi katika mikutano ya kampeni na itakapofika siku ya kupiga kura wawapigie Wagombea wote wanaotokana na CCM.
Naye Mgombea nafasi ya Mwenyekiti katika mtaa wa Mjimwema kupitia Chama cha Mapinduzi Castory Daniel Nditu amewaomba Wananchi kwenda kumchagua yeye pamoja na Wajumbe wake watano ili waweze kushirikiana katika kuleta maendeleo ya pamoja kwenye eneo lao.
Kwa Upande wake Katibu CCM tawi la Mjimwema Ndugu Daniel Manga amewaomba Wananchi katika mkutano huo kuwachagua Wagombea wote waliopendekezwa ndani ya Chama.
Mwenyekiti mstaafu wa Serikali ya Mtaa wa mjimwema Ndugu Fidelis Kisoma,aliwaomba Wananchi kumchagua mrithi wake Castory Daniel Nditu kwa kuwa ni mchapakazi na asiye na makuu na kuwaomba wasisikilize maneno ya uchochezi dhidi yake.