Nuru FM

Moto watekeketeza hekta 400 za miti shamba la Sao Hill Mufindi

19 November 2024, 10:42 am

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Peter Serukamba akiwa katika shamba la SAOHIL kuangalia athari za moto ulioteketeza Miti ya shamba Hilo. Picha na Ayoub Sanga

Na Ayoub Sanga

Hekta zinazokadiriwa kufikia zaidi ya mia nne zimeteketea kwa moto katika mashamba ya Miti ya Sao hill yanayomilikiwa na Serikali pamoja na wananchi yaliyopo Wilaya ya Mufindi , Mkoani Iringa huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.

Akizingumza akiwa katika eneo hilo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Peter serukamba amesema kuwa kwasasa wamesha fanikiwa kudhibiti moto huo huku akipongeza jitihada za Jeshi la zimamoto Mkoa wa Iringa , kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mlale, Sao Hill Mafinga , jeshi la Akiba pamoja na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) .

Sauti ya Serukamba

Aidha RC Serukamba ameyashukuru Majeshi Yote yaliyoshiriki katika kuhakikisha wanauzima moto huo ili usilete madhara makubwa zaidi huku akiwashauri TFS kuwekeza katika zana za kuzima moto.

Sauti ya RC

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Shamba miti la Serikali la Sao Hill PCO Tebby Yoram amesema kuwa eneo kubwa lililo athirika na moto huo ni eneo ambalo tayari limeshavunwa.

Sauti ya Mhifadhi

Moto huo ambao umewaka kwa zaidi ya siku moja umeunguza mashamba hayo jambo lililofanya kuongezwa kwa vyombo vya kuzimia moto kwa wingi ili kudhibiti moto huo usienee maeneo mengine.

MWISHO