DAS Kyando: Tunzeni Miundombinu ya Umeme
1 November 2024, 10:36 am
Na Adelphina Kutika
Wananchi wa Kitongoji cha Itemela na Mpilipili, kata ya Nyazwa, wilayani Kilolo, mkoani Iringa, wamehimizwa kutunza miundombinu ya umeme iliyozinduliwa katika kijiji chao.
Akizungumza baada ya hafla ya uzinduzi wa umeme na utoaji elimu, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Iringa, Mhandisi Grace Ntungi, amesema mradi huu umegharimu milioni 144 za Kitanzania, na akasisitiza umuhimu wa utunzaji wa miundombinu hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya kilolo ,Katibu tawala STOMEN KYANDO ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amewataka wananchi wa vijiji hivyo watumie fursa ya kuweka umeme kwa bei iliyopo kwa sasa kabla miongozo na sera hazijibadilika
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa kata ya Nyazwa BONIPHASI NGWALE ame toa ombi kwa Tanesco, akitaka kuwepo kwa uboreshaji wa miundombinu ya umeme ili kuongeza fursa za kimaendeleo katika kijiji cha Nyazwa.
Hata hivyo Hii ni fursa muhimu kwa wananchi wa Nyazwa, na ni muhimu kwa kila mmoja kutunza miundombinu hiyo ili iweze kuleta maendeleo endelevu.
MWISHO