Nuru FM

Mgogoro wa Wakulima na wafugaji Pawaga kutafutiwa suluhu

19 October 2024, 11:32 am

Wakulima na Wafugaji Tarafa ya Pawaga Wilaya ya Iringa wakizungumza kuhusu Changamoto zao. Picha na Joyce Buganda

Changamoto na kero zinazowakabili wafugaji na wakulima katika Tarafa ya Pawaga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa zimeanza kutatuliwa.

Na Joyce Buganda

WAKULIMA wa Tarafa ya Pawaga, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wamelalamikia vitendo vinavyofanywa na wafugaji kuruhusu mifugo kuingizwa kwenye mashamba ya wakulima bila makubaliano hatua inayochochea ugomvi miongoni mwao.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Ilolo Mpya Fundi Mihayo katika mkutano wa Wafugaji mbele ya mkuu wa wilaya ya Iringa na kueleza kuwa historia inayosababisha kuibuka kwa migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji katika tarafa hiyo ni mipaka ya viwanja.

Sauti ya Diwani

Aidha  Diwani Mihayo amesema kuwa kutokana na uboreshwaji wa miundombinu ikiwemo skimu za umwagiliaji Wafugaji na Wakulima wameongeza hivyo waliwahi kuiomba serikali kupitia ngazi mbalimbali kuangalia eneo jirani na hifadhi ya Taifa ya Ruaha wapewe wafugaji wakubwa na huku Wafugaji wadogo wakibakia ndani ya Tarafa ya Pawaga.

Sauti ya Diwan

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya iringa kheri james amesema wa Wilaya amesema  lengo kubwa ili kutafuta suluhu ya migogoro inayoibuka kati ya Wafugaji na Wakulima kwa siku za nyuma na hivi karibuni.

Sauti ya DC Iringa

MWISHO