SHIUMA lataka machinga Iringa kukomesha migogoro
12 October 2024, 7:45 pm
Na Adelphina Kutika
Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) limewataka wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga mjini Iringa kukomesha migogoro inayowagawa ili wawe na sauti moja katika kushughulikia masuala yao.
Wito huu umetolewa na Katibu Mkuu wa SHIUMA Taifa, Venatus Magaye, katika kongamano la uzinduzi wa kampeni ya Mama nivushe 2025 lililofanyika katika ukumbi wa Highlands Hall, Manispaa ya Iringa ambapo amekiri kuwepo kwa tofauti kati yake na Naibu Katibu Mkuu wa SHIUMA Taifa, Joseph Mwanakijiji, ambaye pia alikuwa kiongozi wa Machinga Iringa.
Kwa uapande wake Joseph Mwanakijiji amesisitiza umuhimu wa umoja miongoni mwa machinga wa Iringa, akisema kuwa ni muhimu kujitahidi pamoja ili kunufaika na fursa nyingi na mipango ya serikali inayowalenga.
Nao baadhi ya machinga waliohudhuria kongamano hilo wamefurahishwa na viongozi hao kuelewana kwani itasaidia kundi hilo la machinga kuwa na umoja na mshikamano utakaowapa fursa za maendeleo.
MWISHO