Bilioni 1.6 kujenga shule ya elimu ya amali Mafinga Mji
26 September 2024, 9:45 am
Na Hafidh Ally
Zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Umma inayotoa elimu ya Amali (Ufundi) katika kata ya Changarawe Halmashauri ya Mafinga Mji mkoani Iringa.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba katika ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Miradi Mjini Mafinga ambapo amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejizatiti kutatua tatizo la ujinga nchini kwa kuwekeza fedha nyingi kwenye Elimu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa amebainisha kuwa watahakikisha wanasima utekelezaji wa Miradi hiyo kabla ya tarehe 31 mwezi wa kumi iwe imekamilika.
Naye Mkurugenzi wa Halmashuri ya Mafinga Maji Bi. Fidelika Myovela amesema kuwa anaishukuru serikali kwa kuwapatia zaidi ya Bilion 3.35 kwa ajili ya shule za sekondari jambo ambalo litasaidia kukuza sekta ya elimu.
Akizungumzia utekelezaji wa Miradi hiyo, Mhandisi wa halmashauri ya Mafinga Mji Bw. Christopher Nyamvugwa amebainisha kuwa wamekuwa wakipata ushirikiano kutoka kwa viongozi wa halmashauri hiyo jambo linalopekelekea miradi ikamilike kwa wakati.
MWISHO