Nuru FM

RC Serukamba aagiza Afisa Manunuzi Iringa DC kusimamishwa kazi

24 September 2024, 10:25 am

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba akitoa maagizo kusimamisha kazi kwa Afisa manunuzi. Picha na Ayoub Sanga.

Na Ayoub Sanga Na Hafidh Ally

Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Peter Serukamba amemuagiza katibu Tawala Mkoa wa Iringa kumsimamisha kazi Afisa manunuzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kushindwa kusimamia kitengo chake na kupelekea miradi inayotekelezwa katika Halmshauri hiyo kusuasua.

Serukamba ametoa Maagizo hayo alipokuwa akikagua miradi ya Elimu yakiwemo madarasa na mabweni na kushangazwa na hatua ya miradi hiyo ilipofikia ambapo miradi hiyo ipo katika hatua ya awali ya msingi.

Sauti ya RC Iringa

Aidha Serukamba mesema kuwa anashangaa kuona fedha zimetolewa na serikali lakini kazi hazifanyiki jambo linalopelekea miradi hiyo kusuasua.

Sauti ya RC Iringa

Akiwa kwenye ukaguzi huo Mhe. Serukamba amemuagiza RAS kuhakikisha wanapata fundi mtu mwingine wa manunuzi ili wapatikane mafundi watakaosimamia miradi kwa manufaa ya wanairinga.

Sauti ya RC Iringa

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi wa Sita Serikali ilitoa fedha kwaajili ya ujenzi wa miradi ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni moja ya Halmashuri iliyopokea fedha nyingi kuliko Halmshuri zingine.

MWISHO